<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><hymn_number>45</hymn_number>
<lyrics>[V1]
 Mtazame Huyo! Aliyeangikwa Hivi sasa upate ishi. Mwenye dhambi dhaifu mtazame tu Wala usifanye tashwishi.

[V2]
 Tazama! Tazama! Tazama uishi!
 Mtazame, Mtazame huyo aliyeangikwa juu
 Hivi sasa upate ishi.

[V3]
 Kama mwana kondoo hakuondoa dhambi,
 Na makosa yako maovu!
 Kama deni zetu zote hakulipa
 Mbona imemwagika damu?

[V4]
 Si kutubu na sala ikomboayo,
 Ila damu ndiyo salama;
 Na aliyeimwaga aweza, sasa,
 Dhambi zako kukufutia.

[V5]
 Usiwe na shaka, Mungu amesema,
 Hakuna alilolisaza;
 Hapo alipokuja alitimiza
 Kazi zote alizoanza.

[V6]
 Basi twae uzima, kwa kufurahi
 Upokee kwa Bwana, sasa;
 Ujijue hakika kwake kuishi
 Yesu aishiye kabisa.</lyrics>
<title>Mtazame Huyo! Aliyeangikwa Juu TZR45</title>
</song>